Pages

August 31, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 30. 08. 2013.
WILAYA YA  MBARALI – AJALI YA  GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
                                             NA   KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 29.08.2013 MAJIRA YA  SAA 18:30HRS HUKO KATIKA KJIJI CHA MWAPIMBUKA  BARABARA YA  MBEYA/IRINGA WILAYA YA  MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI T.877 CLX/T.242 CLV AINA YA  IVECO LIKIENDESHWA NA HABIBU S/O HASSAN, MIAKA 28, MLUGURU, MKAZI WA BUGURUNI DSM, LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO PASTO D/O FURAHA, MIAKA 11, MNYIHA,MWANAFUNZI S/MSINGI IGURUSI DARASA LA PILI MKAZI WA KIJIJI CHA MWAPIMBUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA CHAKE WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA KITUO CHA AFYA IGURUSI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA KITUO HICHO CHA AFYA. CHANZO MWENDO KASI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA KULITELEKEZA GARI  ENEO LA TUKIO MARA  BAADA YA   AJALI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.
WILAYA YA  MBARALI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI
                                             [GONGO] NA   MTAMBO WA KUTENGENEZEA POMBE.
MNAMO TAREHE 29.08.2013 MAJIRA YA  SAA 08:00HRS HUKO RUJEWA MJINI WILAYA YA  MBARALI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA EZEKIEL S/O JAKOBO, MIAKA 26, MBENA,MKULIMA MKAZI WA UHAVILA NA WENZAKE SITA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 25 PAMOJA NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE HIYO. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI NA WAUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.
[ DIWANI ATHUMANI – ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.